Pisi Kali Ligi Kuu Wanawake

WADAU wa soka siku hizi wameanza kuvutiwa na Ligi Kuu ya Wanawake huku na kule kumbe ni kwa sababu ya kuwatazama warembo wanavyojua kusakata soka. Sio Ulaya tu ambako ‘pisi kali’ zimekuwa zikipagawisha mashabiki.

Kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa alikuwepo mrembo aliyeitwa Kosovare Asllani, raia wa Sweden, unaweza kusema huyu alifuata nini kwenye soka - mbona ni pisi kali ambayo inaweza kuwekwa ndani kuliko kuhangaika uwanjani?

Asllani humwambii kitu kuhusu soka amecheza mchezo huo kwa zaidi ya miaka 10 na kupita klabu kadhaa kubwa ikiwemo Manchester City na hadi kufika Real Madrid ya Hispania, na anajua kujitunza na urembo wake ndio maana ukimuona kwa sasa akiwa na miaka 31 hajachakaa.

Sio sawa kuchukulia mchezo wa soka kwa wanawake ni kichaka cha kufanya mambo yasiyofaa kwa jamii, inapaswa kuchukuliwa kama kazi nyingine. Ukiachana na Asllani hizi hapa pisi kali kwenye Ligi ya Wanawake Bara.


1. EVA JACKSON

Advertisement

Amekuwa akifanya vizuri na Ruvuma Queens licha ya kucheza nafasi ngumu golini. Amekuwa akionyesha ubora wake kwa kumudu patashika za washambuliaji mbalimbali wakubwa kwenye ligi hiyo kama vile Opah Clement.


2. FETTY DENSA

Ni beki wa kulia wa Simba Queens ambaye pia amekuwa akiitwa mara kwa mara timu ya taifa ya Wanawake.


pisi pic 1

Kule Segerea ambako ndiko kambi ya klabu yake ilipokuwa amekuwa kivutio kwa mashabiki wengi wa timu hiyo ambao wanatamba kuwa kikosi chao kinaundwa na warembo.


3. PROTASIA MBUNDA

Ruvuma Queens ni miongoni mwa timu kwenye ligi hiyo ambayo imebarikiwa kuwa na Warembo wengi kwenye kikosi chao na Protasia Mbunda ambaye ni beki wa kushoto ni miongoni mwao. Licha ya urembo wake kazi anaiweza uwanjani kwani hapitiki kirahisi na washambuliaji wanaisoma namba.


4.IRENE KISISA

Yanga Princess hawapo nyuma kama warembo wanao kwenye kikosi chao.


pisi pic 3

Irene Kisisa ambaye amekuwa pia akiitwa na kucheza timu ya taifa ya Wanawake amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake ambayo inaongoza msimamo wa ligi. Kwake bora upite mpira halafu mshambuliaji abaki.


5. MEENA BILARY

Kuanzia sura hadi umbo beki huyu wa Yanga ni mashaallah. Yupo zake kwa Wananchi huko Jangwani akitafuta riziki na kupigania ndoto za kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa kike.


pisi pic 2

Amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu na maelewano yake na Kisisa yamekuwa na matunda.


6. STUMAI ABDALLAH

Huwezi kuzungumzia warembo kwenye ligi hiyo halafu ushindwe kumzungumzia Stumai Abdallah kama pisi kali. Mchezaji huyo wa JKT Queens analijua soka kwelikweli na amekuwa akifanya vizuri.


7. TABAGO MWAMVITA

Ni mzuri akishambulia kutokea pembeni, nyota huyo wa Mlandizi Queens amekuwa akiwapagawisha mashabiki wa timu hiyo. Mabeki wamekuwa wakiipata kutokana na kasi aliyonayo, amekuwa na shauku ya kupiga hatua zaidi.


8. JOELLE BUKURU

Ukizungumzia warembo wa kike wa kigeni ambao wanacheza soka nchini bila shaka nambari moja anaweza kuwa Joelle kutoka Burundi. Ni fundi hasa awapo uwanjani na amekuwa akinogesha kikosi cha Simba Queens kwenye eneo la kiungo. Huyu unaweza kusema ni pisi kali na nusu.


9.PHILOMENA KIZIMA

Ni Mrembo mwingine kati ya wachezaji kutoka Yanga Princess ambao ni miongoni mwa pisi kali. Ukimwona unaweza kukubali kuwa hakika halikuwa kosa la kiufundi kumteua. Philomena ana mabao matano kwenye ligi.


10. OPAH CLEMENT

Licha ya kuwa mrembo ila ni kiboko ya makipa kwenye ligi hiyo akiwa na mabao 20 sawa na Fatuma Mustafa wa JKT Queens.

pisi pic

Opah amekuwa akifanya vizuri na timu ya Simba Queens na hata timu ya taifa.


11. ELIZABETH DISMAS

Nyota wa Kigoma Sisterz mwenye uwezo wa kucheza winga ni kati ya wachezaji warembo wanaocheza ligi hiyo. Huko Kigoma unaambia mashabiki ambao wamekuwa wakipata nafasi ya kuangalia mazoezi ya timu hiyo inadaiwa wamekuwa wakimmezea mate.


KOCHA: EDNA LEMA

Yanga Princess inajivunia kuwa na Edna Lema, kocha wa mpira mwenye kujua namna ya kukaa na wachezaji wa kike na kuwajenga kisaikolojia ndio maana licha ya uchanga wa timu hiyo kwenye ligi wanatingisha.

pisi pic 5

Anaweza kuipa Yanga Princess ubingwa kama wachezaji wake wataendelea kujituma kwenye michezo ya ligi kama ilivyo sasa. Edna amekuwa akitumika pia kwenye timu mbalimbali za taifa kwa wanawake.



Post a Comment

0 Comments