Rais Donald Trump wa Marekani hii leo amewaita waandamanaji wanaopinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd katika mji wa Minneapolis kuwa ni "vibaka" na kuonya kwamba watafyatuliwa risasi iwapo wataanza kupora.
Mapema, Trump alielezea kusikitishwa na kifo hicho akisema lilikuwa ni tukio la kushtusha mno. Hata hivyo, alibadilika baada ya machafuko hayo ya jana usiku na kusema kuwa vibaka hao wanachafua kumbukumbu ya Floyd na hatakubali hali hiyo kutokea.
Alisema amezungumza na gavana Tim Walz na kumueleza kwamba jeshi liko upande wake, na iwapo wataanza uporaji wafyatuliwe risasi.

0 Comments
+255717114144