Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya watu kusafiri na kuingia au
kutoka katika mji wa Nairobi na miji mingine minne kwa muda wa siku 21.
Bwana
Kenyatta pia ameongeza tena muda wa amri ya kutotoka nje kuanzia saa
moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri kwa siku 21 zaidi.Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza marufuku ya kuingia na kutoka katika kaunti za Nairobi, Kilifi, kwale Mombasa huku taifa hilo sasa lina maambukizi mapya ya wgonjwa saba na kufanya Kenya kuwa na visa 343 na wagonjwa waliopona ni 98.
Marufuku hii imetangazwa baada ya ile iliyotolewa siku 21 zilizopita kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Rais Kenyatta akanusha madai ya chanjo ya majaribio ya corona kufanyiwa Kenya
Hali ya Corona nchini Kenya ikoje?
Japo amesema kuwa kumekua na mafanikio katika juhudi za kudhibiti ugonjwa, ingawa bado baadhi ya watu hawajaweza kuzingatia ushauri unaotolewa ili kuzuia maambukizi.Wakati huohuo amesema hatua zaidi zitachukuliwa kuhusu kaunti za Mandera, kilif, kwale na Mombasa kwa ushauriano na magavana wa kaunti hizo.
Hivi karibuni idadi ya maambukizi imekua ikiendelea kuongezeka katika katika kaunti ya Mombasa.
Akizungumzia jukuhusu hatua za kukabiliana na athari za janga la corona Bwana Kenyatta amesema Jumatano serikali itaanzisha awamu ya kwanza ya mipango ya kitaifa ya usafi ambayo amesema itasaidia kutoa ajira hususan kwa vijana.
Mipango hiyo inatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 26,000 na baadae awamu nyingine za mipango hiyo zitaendelea na kutoa ajira zaidi.
Amesema usaidizi wa shirilingi bilioni 8 tayari umekwishaanza kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia raia wanaoishi walio katika hatari zaidi ya kupata maambukizi hususan katika makazi duni katika kaunti 7 zilizoathiriwa zaidi.
- Jinsi vipimo vya kugundua virusi vya Corona vinafanya kazi?
- Je unaweza kufanya mazoezi kipindi cha virusi vya Corona?
- Dawa ya corona yashindwa jaribio la kwanza
- Kuvaa barakoa kila mara wanapokua katika maeneo ya umma
- Kunawa mikono kwa sabuni
- Kuendelea kuepuka kukaribiana na kuzingatia ushauri wa kukaa mita mbili kutoka kwa mtu mwingine
- Wasiwaweke hatarini watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na wenye magonjwa ya kudumu
- Amewataka mafundi wa nguo kutengeneza barakoa nyingi na akasema maafisa wa afya watawaelekeza namna zinavyotengenezwa.
- Gari lolote la mizigo halitaruhusiwa kuwa na watu zaidi ya watatu na inapaswa kuwa na kibali cha maafisa
- Usafirishaji wa chakula utaendelea kama kawaida
Wizara ya afya nchini humo ilitangaza wazi kuwa kwamba inatengeneza barakoa ambazo zitasambazwa kwa wananchi hivi karibuni.
Wizara ya afya imeeleza kuwa watu watakaokufa kutokana na virusi vya Corona watazikwa ndani ya saa 24 huku watu wa karibu wa familia wasiozidi 15 wakiruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayoandaliwa na Serikali.
Aidha, ndege kutoka nchi za kigeni zimeendelea kipigwa marufuku kuingia Kenya kwa siku 30 zaidi.
Hatahivyo, marufuku hii iliondolewa kwa ndege za kigeni zinazokuja kuhamisha raia wa nchi za nje waliokwama ingawa zinatakiwa kutoa taarifa kwa serikali angalau saa 72 kabla.
Ndege zingine ambazo hazitaathirika na marufuku hii ni zile za kubeba mizogo hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa serikali inaagiza vifaa vya wahudumu wa afya kutoka nje.
Na kutokana na ongezeko hilo, kuanzia Jumatatu, matatu au daladala pamoja na bodaboda ambazo zitakiuka sheria zilizowekwa zitapokonywa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kusambaza virusi kimaksudi.

0 Comments
+255717114144