Chama cha soka nchini Uholanzi kimetangaza rasmi kuufuta msimu wa
Ligi Kuu Uholanzi 2019/20 na hakutakuwa na Bingwa wala timu ya kushuka
daraja.
Uholanzi wameamua kufuta msimu huo baada ya Waziri Mkuu
wa Uholanzi kutangaza kuahirisha shughuli yoyote ya kimichezo hadi
September 2020 sababu ya virusi vya corona.
Hata hivyo Uholanzi
wamelazimika kufanya hivyo baada ya kuona kuwa hata wakisema wasubiri
hadi September haitakuwa na maana kwani watatakiwa kuwa wameanza msimu
mpya.

0 Comments
+255717114144