Watu wawili waliopatikana na visusi vya coronavirus ni wale waliotangamana na mgonjwa wa kwanza, ambao kwa sasa wametengwa katika chumba maalum kilichopo katika hospitali kuu ya kitaifa ya Kenyatta .
Idadi hii inafanya idadi ya visa vya coronavirus nchini Kenya kufikia watu watatu. Hata hivyo amesema wagonjwa wako katika hali nzuri na hilo linatupa matumaini.
- Jinsi coronavirus inavyoisaidia filamu ya zamani kutazamwa sasa
- Je, ni taarifa gani feki zinazoenezwa Afrika kuhusu coronavirus?
Akizungumza na umma wa Wakenya moja kwa moja kupitia televisheni rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesema masomo katika shule taasisi zote yamesimamishwa mara moja.
Shule za msingi na sekondari zitafungwa kuanzia Jumatatu na za bweni zitafungwa ifikapo Jumatano , amesema rais Kenytatta.
Vyuo vikuu na vyuo pamoja na taasisi nyingine za elimu zitafungwa ifikapo Ijumaa na pale inapowezekana waajiriwa wanapaswa kuruhusiwa kuhfanya kazi nyumani kwao ili kuepukana na maambukizi ya coronavirus.
Amesema watu wote walioingia Kenya raia au wageni watatakiwa kujitenga kwa muda wa siku 14 na yeyote atayekuwa na joto la juu la mwili ajipeleke kwenye kituo cha afya.
Kulingana na tamko la rais huyo ni raia wa Kenya tu na wakazi wa kigeni wenye visa halali watakaokubaliwa kuingia nchini Kenya kwa muda wa siku 30 zijazo ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.
''Ili kuepuka maambukizi kwa njia ya pesa tunashauri watu watumie njia ya matumizi ya pesa ya mobile, credit bank, na tunazitaka benki ziangalie jinsi ya kupunguza viwango tozo za matumizi ya simu za mkononi ya pesa'', amesema Bwana Kenyatta ambaye amewataka Wakenya kuwa watulivu.
Huku akiainisha agizo lake hilo kwa vipengele Bwana Kenyatta amesema kwa mujibu wa agizo la kuepuka maeneo yenye mikusanyiko mikubwa, watu waepuke maeneo yenye umati wa watu, agizo lake likisema watu :
- waepuke mikusanyiko ikiwemo maeneo ya kuabudu
- wapunguze mikusanyiko ya kijamii mkiwemo harusi na mazishi, na masharti hayo yazingatiwe na mara moja na wanafamilia
- waepuke maeeno mkiwemo maduka ya jumlana maeneo ya burudani
- wapunguze mikusanyiko katika maeneo ya usafiri wa umma na kwingineko iwezekanavyo.
- Kuwepo ukomo wa wageni wanaotembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali za umma na za kibinafsi.

-
Awali Sekta ya mahakama nchini Kenya imechukua hatua ya kufunga baadhi ya shughuli zake kufuatia taarifa ya kupatikana kwa mtu wa kwanza mwenye virusi vya corona nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jaji Mkuu nchini humo David Maraga amesema kuwa mahakama inasitisha uendeshaji wa kesi ndogondogo mwa muda wa siku 14.
Aidha amesema kuwa wafungwa waliopo rumande hawatafikishwa mahakamani na badala yake wenye makosa madogo madogo watatozwa faini katika kituo cha polisi, kulingana na mwongozo utakaotolewa na Kamishna Mkuu wa polisi.
Amesema kuwa majaji hawatapewa mafunzo kwa kipindi cha siku 14 na safari za nje ya nchi zimesitishwa.
Tangazo hili limetolewa na Rais Kenyatta huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutanda nchini humo tangu kutangazwa kwa kisa cha kwanza cha mlipuko wa coronavirus, huku baadhi ya wakazi wa jiji la Nairobi wakionekana kununua bidhaa kwa wingi kwa hofu ya kuzikosa baadae iwapo mlipuko utaendelea kusambaa.

0 Comments
+255717114144